LIGI KUU VODACOM iliendelea kwenye Viwanja tofauti.
Ndanda wakicheza nyumbani nangwanda sijaona wameshindwa kutamba baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prison
Huko Manungu, Morogoro, Timu iliyoanza kwa kishindo na kuporomoka ghafla, Mtibwa Sugar imeitokka sare ya 1-1 na Mabingwa Watetezi Azam FC katika Mechi muhimu mno kwa kila upande goli la Mtibwa lilifungwa na Mussa Mgosi na lile la azam likifungwa na Himid Mao
Azam FC, wanabaki Nafasi ya Pili, Pointi 5 nyuma ya Vinara Yanga, wanasaka ushindi ili kulitetea Taji lao lakini Mtibwa walioporomoka hadi mkiani Nafasi ya 12 wanawania kujinusuru kushuka Daraja.
![]() |
COAST UNION |
Mechi nyingine ya iliyokuwa na mvuto ni ile ya Coastal Union ambapo wakiwa ugenini leo wameitandika Ruvu JKT. magoli 2-0 magoli yaliyofungwa na Ike Obinna na Rama Salim katika mchezo uliopigwa Azam Complex, Chamazi, Viunga vya Jiji la Dar es Salaam
Siku ya Jumapili zipo Mechi mbili na Vinara wa Ligi Yanga wako Nyumbani Uwanja wa Taifa kucheza na Mbeya City ambayo iko Nafasi ya 7.
0 comments:
Post a Comment