Pages

Friday, 10 April 2015

VITA YA LIGI KUU BARA KESHO NA KESHOKUTWA NDANDA KUWAKARIBISHA VIBONDE PRISON BIG MECHI AZAM VS MTIBWA



Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika viwanja sita tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho Jumamosi, na michezo miwili kuchezwa siku ya jumapili.
KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR
Jumamosi JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Manungu-Turiani mjini Morogoro,nayo  Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
KIKOSI CHA NDANDA FC YA MTWARA

Ligi hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, huku mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya Stand United wakiwakaribisha maafande wa  timu ya Polisi Morogoro.


RATIBA KAMILI YA LIGI KUU

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates