Christiano Ronaldo amefutiwa Kadi ya Njano aliyopewa Juzi wakati Real Madrid inaifunga Rayo Vallecano na sasa yuko huru kucheza Mechi ya La Liga Jumamosi na Eibar.
Kadi ya Njano hiyo ilikuwa Kadi yake ya 5 na hivyo kumfanya afungiwe Mechi 1 lakini Klabu yake Real ilikata Rufaa kupinga Kadi hiyo iliyotolewa wakati Ronaldo alipochezewa Rafu ya wazi na kunyimwa Penati lakini Refa alimhukumu kuwa amejiangusha kusudi na kumpa Kadi ya Njano Ronaldo na kuwanyima Penati.
Mara baada ya Mechi hiyo, Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, alisema huo ni uonevu na watakata Rufaa ambayo sasa imekubaliwa na Kadi hiyo kufutwa.
Sasa ni wazi Ronaldo ataanza Mechi ya La Liga ya Jumamosi Uwanjani Santiago Bernabeu na Eibar ambayo Ronaldo anawania kupiga Bao lake la 301 kwa Real baada ya Juzi kufikia Bao 300.
Lakini kwenye Mechi hii na Eibar, Real itawakosa Mastaa wao wawili, Toni Kroos na James Rodriguez, ambao wapo Kifungo cha Mechi 1 baada ya kulimbikiza Kadi za Njano 5.
Hata hivyo pengine hilo ni baraka kwa Real kwani kati ya Wiki ijayo wana Mechi kali ya Dabi ya Madrid dhidi ya Atletico Madrid ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
0 comments:
Post a Comment