Kikosi cha wakongwe wa Barcelona kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya nyota wakongwe wa Tanzania katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliaji Patrick Kluivert ndiye alikuwa shujaa baada ya kufunga mkwaju wa penalti wa bao la pili.
Kluivert alifunga mkwaju huo na kumuacha kipa Juma Kaseja akianguka kushoto kwake na mpira ukiingia kulia.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Luis Garcia ambaye aliwachambua mabeki wa Tanzania wakongwe na kufunga.
Yusuf Macho ‘Musso’ akafunga baso safi la pili kwa shuti kali katika dakika ya 42. Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko.
Hadi dakika 90 zinamalizika Barcelona 2 Tanzania eleven 1
0 comments:
Post a Comment