Mechi 5 za Ligi Kuu England zimeleta msisimko baada ya kushusha Magoli kibao na mengine kufungwa mwishoni.
Bao la Dakika ya 12 la Aaron Ramsey limewachimbia Arsenal Nafasi ya Pili ya Ligi Kuu England walipoifunga Burnley Bao 1-0 Ugenini.
Arsenal sasa wako Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wana Mechi 2 mkononi na Leo wanacheza Ugenini na QPR.
Arsenal pia wameiacha TImu ya Tatu Man United kwa Pointi 4 ambao lao wako kwao Old Trafford kucheza na Mahasimu wao Man City.
*****************
Huko White Hart Lane, Christian Benteke wa Aston Villa aliwanyamazisha Wenyeji Tottenham kwa kufunga Bao pekee na la ushindi katika Dakika ya 35 kwenye Mechi ambayo Villa walimaliza Mtu 10 baada ya Carlos Sanchez Moreno kutolewa mwishoni kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano 2.
******************
Southampton, wakicheza Nyumbani, waliichapa Hull City Bao 2-0 kwa Bao za James Ward-Prowse, kwa Penati, na Graziano Pele.
******************
Huko The Hawthorns, Wenyeji West Bromwich Albion walichapwa 3-2 na Timu ya Mkiani Leicester City ambayo Bao lake la 3 na la ushindi lilifungwa Dakika za Majeruhi na James Vardy.
Bao nyingine za Mechi hiyo zilifungwa na Fletcher na Craig Gardner kwa WBA na David Nugent na Huth kwa Leicester.
*****************
Upton Park nayo pia ilishuhudia Bao la Dakika ya 90 wakati Marco Arnautovic alipoisawazishia Stoke City iliyotanguliwa na West Ham kwa Bao la Dakika ya 7 la Aaron Cresswell.
*****************
Huko Stadium of Light, Wenyeji Sunderland walibamizwa 4-1 na Crystal Palace ambayo ilifunga Bao zake kupitia Glenn Murray na Hetitriki ya Yannick Bolasie huku Bao la Sunderland likifungwa Dakika ya 90 na Connor Wickham.
MATOKEO YA MECHI ZOTE
Swansea 1 Everton 1
Southampton 2 Hull 0
Sunderland 1 Crystal Palace 4
Tottenham 0 Aston Villa 1
West Brom 2 Leicester 3
West Ham 1 Stoke 0
Burnley 0 Arsenal 1
RATIBA YA MECHI ZA LEO
Jumapili Aprili 127
530 QPR v Chelsea
1800 Man United v Man City
Jumatatu Aprili 13
2200 Liverpool v Newcastle
0 comments:
Post a Comment