Pages

Tuesday, 7 April 2015

TETES ZA USAJILI ULAYA ADEBAYOR KUONDOKA SPURS, FALCAO KWENDA LIVERPOOL

EMMANUEL ADEBAYOR
Wakati ambapo Spurs inapambana kufuzu kwenye Europa League, mshambuliaji Emmanuel Adebayor, 31, ataongoza orodha ya wachezaji kadhaa kuondoka White Hart Lane. Mlinzi Younes Kaboul, 29, na viungo Etienne Capoue na Paulinho, wote 26, wanataka kuuzwa. 


RADAMEL FALCAO
Klabu ya Anfield ipo kwenye mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya mshambuliaji Radamel Falcao, ambaye yupo klabuni hapo kwa mkopo akitokea Monaco, wakitaka kumsainisha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia, 29 kwa mkopo msimu ujao. 


MAXIMILIANO ROMERO


Arsenal wanakaribia kumnasa mchezaji wa kimataifa wa Argentina Maximiliano Romero kutoka Velez Sarsfield kwa ada ya paundi 4.5m. Romero, 16 anatajwa kuwa 'Lionel Messi ajaye'.

Kiungo wa Chelsea Oriol Romeu, 23, yupo tayari kuondoka Stamford Bridge wakati wa usajili ujao. Mhispania huyo yupo kwa mkopo kwenye klabu ya Stuttgart msimu huu na ameanza kwenye michezo 15 kwenye kikosi cha Blues tangu alipojiunga akitokea Barcelona mwaka 2011. 



Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates