Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki
katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2018 baada ya
kukataa kumlipa kocha wake wa zamani Jose Claudinei Georgini.
Shrikisho la soka FIFA limesema katika taarifa kwamba limechukua hatua hiyo baada ya taifa hilo kushindwa kumlipa kocha huyo.
Fifa imeongezea kuwa shirikisho la soka nchini Zimbabwe ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo licha ya kupewa mda wa kufanya hivyo.
Marufuku hiyo inakatiza fursa ya taifa hilo kufuzu katika fainali za kombe hilo nchini Urusi kabla ya kuanza harakati zake za kutaka kufuzu.
Mechi za kufuzu kwa dimba hilo barani Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi Octoba huku droo ikifanywa mnamo mwezi Julai mjini St Petersburg.
Zimbabwe haijawahi kufuzu katika mechi za kombe la dunia.
CHANZO: BBC
0 comments:
Post a Comment