Pages

Tuesday, 17 March 2015

FRANSIS CHEKA ATOKA JELA SASA KUTUMIKIA KIFUNGO NJE

Bondia nyota zaidi nchini, Francis Cheka ameachiwa huru, baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani. 
Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro. Lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo. 
“Tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia ishu hiyo. Ila tayari yuko nje,” alisema Kaike Siraju, promota wa ngumi za kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha Cheka anatoka. 
Cheka alipatikana na hatia ya kushambulia baada ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakamani ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alimhukumu kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.
Bondia huyo ambaye amewahi kuwa Bingwa wa Dunia wa mkanda wa WBF alimshambulia aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda, Julai 2, mwaka jana katika Ukumbi wa Vijana Social Hall aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuli za baa zilizokuwa zinasimamiwa na KIbanda.
Kutokana na maamuzi ambayo yamefanyika leo Mkoani Morogoro, Sasa Nyota huyo atakuwa akitumikia muda wake uliobaki akiwa nje huku akijihusisha na dhughuli za kijela za nje.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates