Pages

Tuesday, 10 March 2015

GOLIKIPA JUMA KASEJA SASA KUSAJILIWA NA STAND UNITED

Uongozi wa Stand United ya Shinyanga uko mbioni kukamilisha usajili wa kipa mkongwe Juma Kaseja, NIPASHE imebaini.

  Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu, zilieleza kuwa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo ya usukumani imeagiza Kaseja asajiliwe mara moja kwa ajili ya kuimarisha timu msimu ujao.

"Ni kweli tumeanza mazungumzo na Kaseja na amekubali kujiunga nasi, lakini amesema tumalizane na meneja wake. Jumatano (kesho) tutakuwa na mazungumzo na meneja na tunaamini kila kitu kitakwenda vizuri maana mchezaji ameshakubali," Kanu alisema na kuongeza:

"Kamati ya Utendaji ya Stand imeagiza usajili wetu wa msimu ujao tuanze na Kaseja. Imenikabidhi jukumu hilo nihakikishe ninamnasa Kaseja ili atuongezee nguvu. Kikao chetu na meneja wa mchezaji ndicho kitaamua atakuwa nasi kwa muda gani na kwa fungu kiasi gani."
 
Kaseja, mchezaji wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, kwa sasa hana timu baada ya kutosana na Yanga ambao wameshamfungulia kesi ya madai mahakamani.
 
Hata hivyo, Kaseja alikana kufanya mazungumzo na mtu yeyote wa timu ya 'Chama la Wana'.
 
"Mimi sijazungumza na mtu yeyote kwa sasa kuhusu kunisajili. Kama yeye (Kanu) amekwambia hivyo, basi akueleze kwa kina," alisema Kaseja baada ya kutafutwa na NIPASHE jijini jana.
CHANZO:NIPASHE
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates