Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid, wamechapwa kwao Bao 4-3 na FC Schalke lakini wametinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 5-4.
Katika Kipindi cha Kwanza, ambacho FC Schalke walitawala na kutangulia kufunga mara mbili lakini Cristiano Ronaldo, mara mbili, alifunga Bao za Kichwa na kusawazisha.
Katika Kipindi hiki, Schlake walipata nafasi kadhaa za kufunga na mbili kumwangukia Klaas-Jan Huntelaar ambae kwanza aliinasa pasi ya nyuma ya Varane kwa Kipa na kukosa na kisha kupiga Posti kwa shuti kali.
Kipindi cha Pili, Karim Benzema aliipa Real Bao la 3 na Kijana wa Miaka 19 kutoka Germany, Leroy Sane, aliisawazishia Schalke kwa Shuti safi lililomshinda Kipa Iker Casisallas.
Alikuwa tena Klaas-Jan Huntelaar aliepiga Bao la ushindi baada ya mchezo safi wa Leroy Sane.
Real Madrid sasa imetinga Robo Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-4 na itajua mpinzani wake hapo Machi 20 Droo itakapofanyika.
FC Porto 4 FC Basel 0
FC Porto wameitandika FC Basel Bao 4-0 katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Ureno.
Katika Mechi ya kwanza huko Uswisi, Timu hizi zilitoka Sare ya 1-1.
Mchezaji wa Kimataifa wa Algeria Yacine Brahimi alifunga Bao kwa Frikiki safi ya Dakika ya 14 na kuwafungulia milango FC Porto ambao Kipindi cha Pili, FC Porto walipiga Bao 3 nyingine kupitia Hector Herrera, Frikiki safi ya Carlos Casemiro na Goli la Ruben Neves.
FC Porto imetinga Robo Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-1 na itajua mpinzani wake hapo Machi 20 Droo itakapofanyika.
0 comments:
Post a Comment