Baada kuchapwa na Manchester United katika Mechi yao ya mwisho iliyopita, Liverpool wamepokea kipigo kingine cha magoli 4-1 pale Emirates na kupoteza matumaini ya kufuzu 4 Bora.
Mbali na kuwa na rekodi mbovu Emirates ambako wameshinda mechi 1 tu Sare 7 na Vipigo 9, Liverpool waliwakosa Nahodha wao Steven Gerrard na Sentahafu Martin Skrtel ambao wako Kifungoni.
Arsenal, baada ya kuyumba mwanzoni mwa Ligi kiasi cha Mashabiki wao kumtaka Meneja wao Arsene Wenger aliedumu Miaka 19 aondoke, walijirekebisha na sasa wanaendelea kubaki Nafasi ya 3.
Magoli ya Arsenal yamefungwa na Bellerin dakika ya 37,Mesut Oezil dakika ya 40, Alexis Sanchez 45, Giroud 90 goli la kufutia machozi la Liverpool lilifungwa na Henderson Dk ya 76
0 comments:
Post a Comment