Wakiwa kwao Nou Camp, FC Barcelona wamefuzu kutinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada kushinda Bao 2-0 na kusonga kwa Jumla ya Mabao 5-1 katika Mechi mbili dhidi ya Paris Saint-Germain ya France.
Barca walipata Bao la Kwanza Dakika ya 14 wakati Neymar alipomalizia pasi safi ya Andres Iniesta.
Alikuwa Neymar tena alieipa Barca Bao la Pili kwa Kichwa kufuatia Krosi ya Dani Alves ya Dakika ya 33.
Hadi Mapumziko Barca 2 PSG 0.
Jumatano Usiku zipo Mechi nyingine mbili za Robo Fainali na Juventus, walioshinda kwao Turin, Italy Bao 1-0, wako Ugenini kurudiana na AS Monaco na pia ipo Bigi Mechi, El Derbi Madrileno, Dabi ya Jiji la Madrid, wakati Mahasimu Real Madrid na Atletico Madrid watakaporudiana huko Santiago Bernabeu huku matokeo ya Mechi ya kwanza yakiwa ni 0-0.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 24 huko Nyon, Uswisi na Mechi zake zitachezwa Mei 5 na 6 na Marudiano hapo Mei 12 na 13.

0 comments:
Post a Comment