Pages

Saturday, 25 April 2015

BUNDESLIGA : BAYERN UBINGWA WA 25 UNANUKIA MECHI ZA WEEKEND HII ZITAAMUA

Bayern Munich, ambao Msimu huu wanakimbiza Mataji Matatu, wanaweza kutwaa Taji lao la kwanza Wikiendi hii kwa kuutetea Ubingwa wao wa Ligi ya Bundesliga na hii itakuwa ni mara 25 kutwaa Ubingwa wa Germany.
Zikiwa zimebaki Gemu 5 na wao wakiwa Pointi 12 mbele ya Timu ya Pili VfL Wolfsburg, Bayern leo hii
watacheza Nyumbani Allianz Arena na Hertha Berlin na watatwaa Ubingwa wakipata matokeo bora kupita ambayo Wolfsburg watayapata Jumapili wakicheza na Ugenini na Borussia Moenchengladbach.
Bayern wapo kwenye wimbi la ushindi baada ya Juzi kuibomoa FC Porto Bao 6-1 Uwanjani Allianz Arena baada kupoteza Mechi ya kwanza 3-1 huko Ureno na sasa wapo Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo watacheza na Barcelona.

Pia Jumanne, Bayern wanacheza Nusu Fainali ya Kombe la Ujerumani, DFB-POKAL, na Borussia Dortmund Uwanjani kwao Allianz Arena.
Hata hivyo, Bayern wanakabiliwa na Majeruhi kadhaa wakiwemo Franck Ribery, Mehdi Benatia na David Alaba lakini upo uwezekano wa Arjen Robben na Javi Martinez kurejea baada kupona.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates