Zikiwa zimebaki mechi 3 tu kuamua timu ya Ndanda ibaki au ishuke daraja leo hii timu hiyo kutoka Mtwara ipo katika vita nzito katika uwanja wa taifa dhidi ya timu kongwe simba sc watakapo menyana baadae hii leo katika mchezo wa ligi kuu vodacom Tanzania bara
Simba inayoshika nafasi ya tatu ikiwa n pointi 38 inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushindi mnono wa mabao 4-0 iliyupata Jumantano iliyopita dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga.
Ndanda timu ngeni ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza ligi ya Vodacom msimu huu mambo yao siyo mazuri sana kwani inashika nafasi pili kutoka ya mwisho ikiwa na pointi 25 .
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na malengo ya timu zote mbili Simba ambayo ni wenyeji wakitaka kupata ushindi ili kujiweka kwenye mazingira ya kumaliza nafasi ya pili wakati Ndanda FC, wakitaka kukimbia kushuka daraja na kulipa kisasi cha mabao 2-0, walichofungwa kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa msemaji wa Simba Haji Manara amesema timu hiyo itamkosa nahodha wake Hassani Isihaka na mshambuliaji wa kiataifa kutoka Uganda Danny Sserunkuma, wanaosumbuliwa na majeruhi huku kipa chaguo la pili Manyika Peter akitarajiwa kuanzia benchi baada ya kumaliza matatizo yake na uongozi.
Kopunovic ameiambia Goal, lengo lao ni kuhakikisha wanashinda mechi zao zote watakazo shuka dimbani na mwisho wa ligi watajua nafasi yao kama nafasi ya pili ama yatatu.
Kocha wa ndanda Major Abdul Mingane amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kesho na hana majeruhi yeyote lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanapambana na kupata pointi zote tatu kwenye uwanja wa taifa na kama ikishindikana angalau pointi moja kwao itakuwa na faida kubwa.*****************************
Nao Azam FC wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kuikwepa Simba ambao wako nyuma yao
****************************
MBEYA CITY VS KAGERA
0 comments:
Post a Comment