Ingawa wapo Nafasi ya 10 wakiwa Pointi 36 nyuma ya FC Barcelona, Espanyol bado ni Mahasimu wakubwa wa Vinara hao wa La Liga na Jumamosi Jiji la Barcelona litajaa shamrashamra za 'El Derbi Barceloni'.
Ingawa pia Msimu huu Barca waliinyuka Espanyol 5-1 ndani ya Nou Camp katika Mechi yao ya kwanza ya La Liga, Uwanjani Estadi Cornella-El Prat, Espanyol huwa habari nyingine na Barca wanajua hilo.
Licha ya kuwa hii ni Dabi na huwa zina kawaida ya kutotabirika, Barcelona wapo kwenye presha ya kushinda ili kuendelea kuongoza Ligi kwani wakitetereka tu nyuma yao kwa Pointi 2 wapo Real Madrid.
******************
0 comments:
Post a Comment