Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye michuano ya Klabu Barani Afrika, Jumamosi watashuka katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Yanga imetua hatua hii baada ya kuzibwaga BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe katika Raundi za awali.
Akizungumza na INFO RADIO,Jana Mkuu wa kitengo cha habari Yanga, Jerry Muro, amesema mmandalizi yako vizuri na timu hiyo imekuwa ikifanya mazoezi asubuhi na jioni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo huku akisema watanzania wasihofie kwani ushindi uko palepale
Yanga inatarajiwa kuwatumia tena Wachezaji wao muhimu ambao walikuwa Majeruhi ambao ni Salum Telela na Coutinho.
Etoile du Sahel inatarajiwa kutua Dar es Salaam Leo hii kwa Ndege ya kukodi.
0 comments:
Post a Comment