Pages

Thursday, 16 April 2015

UEFA BARCELONA YAIUA 3-1 PSG, PORTO NAO WAIFUNDISHA KAZI BAYERN WALIPOINYUKA 3-1


Wakicheza Nyumbani bila ya Staa wao mkubwa Zlatan Ibrahimovic ambae yupo kwenye Kifungo cha Mechi 1, PSG Usiku huu wamekiona cha mtema kuni baada ya kutandikwa Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hadi Mapumziko, Barcelona walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Neymar baada ya kulishwa na Lionel Messi.
Kipindi cha Pili Dakika ya 67 Luis Suarez akaipa Barca Bao la Pili safi mno baada kumtoka David Luiz na kuhadaa Mabeki wawili wa PSG, Marquinhos na Maxwell, na kuachia shuti lililomshinda Kipa Sirigu.

Luis Suarez tena aliifanya Barca iongoze Bao 3-0 baada ya kupachika Bao Dakika ya 78 baada ya tena kuipita ngome ya PSG kirahisi na kupindisha Mpira juu wavuni.
Dakika ya 82 PSG walipata Bao Mfungaji akiwa Fulbeki wao Gregory van der Wiel ambae Shuti lake lilimbabatiza Beki wa Barca Jeremy Mathieu.
Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp Wiki ijayo.

***********************
FC PORTO 3 BAYERN MUNICH 1
Uwanja: Estádio do Dragão, Porto, Portugal
FC Porto wametumia vyema Uwanja wa Nyumbani baada ya kuwachapa Vigogo wa Germany Bayern Munich Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

FC Porto walitangulia kufunga Bao 2 kwa Bao za Ricardo Qaresma na la kwanza lilikuwa katika Dakika ya 3 tu kwa Penati baada ya Kipa Manuel Neuer kumwangusha Jackson Martinez na kulambwa Kadi ya Njano.
Bao la Pili Quaresma alifunga Dakika ya 10 na Bayern Munich kupata Bao 1 katika Dakika ya 28 kupitia Thiago.
Hadi Mapumziko FC Porto 2 Bayern Munich 1.
Kipindi cha Pili, FC Porto walifunga Bao lao la 3 katika Dakika ya 65 Mfungaji akiwa Jackson Martinez.
Timu hizi zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich Wiki ijayo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates