Neymar na Lionel Messi wamefunga Bao 2 za Kipindi cha Kwanza walipocheza Ugenini na Wapinzani wao wa Jadi Espanyol na kuipandisha Barcelona juu zaidi kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Real Madrid.
Bao hizo 2 zilifungwa ndani ya Dakika 8 kwa Neymar kupiga la Kwanza Dakika ya 17 na Messi kufunga la Pili Dakika ya 25.
Mapema Kipindi cha Pili, Barca walibaki Mtu baada ya Jordi Alba kupewa Kadi za Njano mbili mfululizo katika Dakika ya 54 na kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kulalamika kupindukia kwa Refa Mateu Lahoz.
Nao Espanyol walikubwa na balaa hilo hilo katika Dakika ya 90 kufuatia Hector Moreno kulambwa Kadi za Njano mbili na kupewa Kadi Nyekundu kwa kulalamika.
Real Madrid wao wanacheza Jumapili Ugenini na Celta Vigo Timu ambayo waliichapa 3-0 katika Mechi ya kwanza.
Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao Juzi walipigwa 1-0 na Real na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Jumamosi wapo Nyumbani kucheza na Elche wakiwa tayari wameshapoteza matumaini ya kutetea Taji lao.
0 comments:
Post a Comment