Jumanne Usiku itakuwa ni mara ya 4 kwa Barcelona na Paris Saint-Germain kukutana Msimu huu kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na mara ya mwisho Uwanjani Nou Camp, hapo Desemba 10, Barca iliinyuka PSG Bao 3-1 kwen
ye Mechi ya mwisho ya Kundi F la UCL
ye Mechi ya mwisho ya Kundi F la UCL
Safari hii wanakutana ikiwa ni marudiano ya Robo Fainali ya UCL huku Barca wakiwa mbele kwa Bao 3-1 walizoifunga PSG huko Paris Wiki iliyopita.
******************
Mabingwa wa Germany Bayern Munich Jumanne Usiku wako Uwanjani kwao Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany wakisaka kuweka Historia ya kupindua kipigo cha 3-1 walichopewa na FC Porto huko Mjini Porto, Ureno Wiki iliyopita kwenye Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Lakini kazi hii kwao si rahisi kwani Bayern itawakosa Mastaa wao kadhaa kwa Majeruhi na mmoja ni Winga wa France Franck Ribery ambae yuko nje ya Uwanja Mwezi sasa akijiuguza Enka yake.
Kocha wa Bayern, Pep Guardiola, amekiri kuwa ipo nafasi finyu kwa Ribery kucheza Mechi hii.
Lakini, Kiungo wa Germany, Bastian Schweinsteiger huenda akacheza baada ya kuanza tena Mazoezi.
Wengine ambao wataikosa Mechi hii na FC Porto ni David Alaba, Arjen Robben na Sentahafu wa zamani wa AS Roma, Mehdi Benatia.
Akipiga mbiu ya mgambo ya ushindi, Guardiola amesema kutwaa Bundesliga na DFB-POKAL haitoshi kwao bali kutwaa Trebo ndio lengo lao akimaanisha ushindi pia kwenye UCL.
FC Porto watawakosa Wachezaji wao wawili, Alex Sandro na Danilo, ambao wapo Kifungoni.
Baada ya Mechi hizi za Jumanne, Jumatano Usiku, Juventus, walioshinda kwao Turin, Italy Bao 1-0, wako Ugenini kurudiana na AS Monaco na Siku hiyo hiyo ipo El Derbi Madrileno, Dabi ya Jiji la Madrid, wakati Mahasimu Real Madrid na Atletico Madrid watakaporudiana huko Santiago Bernabeu huku matokeo ya Mechi ya kwanza yakiwa ni 0-0
0 comments:
Post a Comment