Aston Villa watakutana na Mabingwa Watetezi Arsenal kwenye Fainali ya FA CUP baada ya kutoka nyuma na kuitandika Liverpool Bao 2-1 katika Mechi ya Nusu Fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembley Jijini London.
Arsenal, kwenye Nusu Fainali nyingine, walitumia Dakika 120 kuifunga Timu ya Daraja la chini Reading Bao 2-1 na kutinga Fainali.
Liverpool, wakiongozwa na Nahodha wao Steven Gerrard ambae kumbukumbu ya Siku yake ya Kuzaliwa ni Mei 30 Siku ya Fainali ya FA CUP kitu ambacho Liverpool walikiota kitatokea Gerrard kubeba Kombe, ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 30 la Philippe Coutinho aliepokea pasi ya Raheem Sterling lakini Dakika 6 baadae Straika wa Aston Villa Christian Benteke alisawazisha Bao hilo baada ya kuikamata pasi safi ya Fabian Delph.
Hadi Mapumziko Aston Villa 1 Liverpool 1
Kipindi cha Pili, Dakika ya 54, Fabian Delph alianzisha muvu safi na kumpa Benteke aliemsogezea Grealish aliemrudishia Fabian Delph na kupiga Bao la Pili safi na la ushindi.
Fainali ya FA CUP itachezwa Mei 30 Uwanja wa Wembley.
0 comments:
Post a Comment