Baada ya vichapo viwili mfululizo toka kwa Crystal Palace na Manchester United, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City Leo kwao Etihad wamezinduka na kuichapa West Ham Bao 2-0.
Ushindi huu umewachimbia City Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Man United na kuiacha Liverpool, iliyo Nafasi ya 5, kwa Pointi 7.
Bao za City zilifungwa na Beki wa West Ham James Collins aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 18 alipojaribu kuokoa Krosi ya Jesus Navas na la pili kufungwa Dakika ya 36 na Sergio Aguero baada ya kaunta ataki safi iliyoanzishwa na Yaya Toure kuunasa Mpira na kucheza na Aguero aliempa Navas na kurudishiwa tena na kufunga.
0 comments:
Post a Comment