Pages

Sunday, 19 April 2015

LA LIGA: MASTAA WATENGENEZA REKODI MESSI AFIKISHA GOLI LA 400 NAE RONALDO GOLI LA 50 MSIMU HUU BARCA,REAL WOTE USHINDI

Vigogo wa Spain, Barcelona na Real Madrid, jana wameendelea kufukuzana katika mbio za Ubingwa wa La Liga baada ya wote kushinda Mechi zao huku Masupastaa wao wakubwa, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, wakiweka Rekodi mpya.

Barcelona, wakicheza kwao Nou Camp, waliichapa Valencia 2-0 kwa Bao za Luis Suarez na Lionel Messi ambae sasa amefikisha Bao 400 kwenyecLa Liga akiwa na Barca.
Katika Mechi hiyo ambayo Bao la kwanza la Barca lilifungwa Dakika ya 1 tu na Suarez, Valencia waliipoteza nafasi murua ya kusawazisha katika Dakika ya 10 baada ya kupewa Penati kufuatia Beki wa Barca Gerard Pique kumchezea faulo Rodrigo Moreno lakini Penati hiyo iliyopigwa na Dani Parejo iliokolewa na Kipa Claudio Bravo.

Huko Santiago Bernabeu, Real Madrid waliichapa Malaga Bao 3-1 kwa Bao za Sergio Ramos, James Rodriguez na Cristiano Ronaldo ambae pia alikosa Penati.

Bao la Ronaldo, alilotengewa na Javier Hernandez 'Chicharito', ni Bao lake la 50 Msimu huu katika Mechi 45 alizoichezea Real na limemfanya aweke Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza huko Spain kufunga Bao 50 katika Misimu Mitano mfululizo.
Hadi sasa La Liga inaongozwa na Barca walio Pointi 2 mbele ya Timu ya Pili Real Madrid.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates