Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, Leo hii Uwanja wa Wembley Jijini London, wameichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading, Bao 2-1 katika Nusu Fainali ya FA CUP.
Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa Goli.
Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici
Nusu Fainali nyingine ni leo pale Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.
Kabla Mechi hii Katika Mechi 12 zilizopita kati ya Arsenal na Reading, Arsenal wameshinda Mechi zote.
Katika Mechi hizo 12, Arsenal walifunga Bao 37.
0 comments:
Post a Comment