Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, AzamFC, wakiwa kwao Azam Complex, Chamazi, wamefuta balaa ya Sare zilizowaandama na kuichapa Kagera Sugar Bao 2-1.
Ushindi huu umewasogeza Azam FC na kuwakaribia Vinara wa Ligi, Yanga, na sasa wapo Pointi 4 nyuma yao lakini wao wamecheza Mechi moja zaidi.
Mabao katika Mechi hiyo yalifungwa na Frank Domayo kwa Azam FC katika Dakika ya 40 na Kagera Sugar kusawazisha Dakika ya 54 kwa Bao la Babu Ally lakini Gaudence Mwaikimba akaipa ushindi Azam FC kwa Bao lake la Dakika za lala salama.
KIKOSI CHA POLISI MORO KILICHOIANGAMIZA NDANDA JANA |
Huko Morogoro, Polisi Moro waliichapa Ndanda FC Bao 2-0 kwa Bao za Edward Christopher, Dakika ya 64, na Said Bahanuzi, Dakika ya 74.
Huko Sokoine, Mbeya, Wenyeji Mbeya City waliitwanga Simba Bao 2-0 kwa Bao za Paul Nonga katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza na la pili kufungwa na Peter Mwalyanzi katika Dakika ya 69.
Jumapili kuna mechi mbili huko Mabatini, Mlandizi kwa Wenyeji Ruvu Shooting watakapocheza na Mgambo JKT na Sokoine Mbeya ni Tanzania Prison na Mtibwa
Hadi sasa Yanga ndio wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 4 mbele ya Mabingwa Watetezi Azam FC ambao wamecheza Mechi moja zaidi.
0 comments:
Post a Comment