Liverpool wapo Nafasi ya 5 Pointi 7 nyuma ya Man United na Leo Jumatano wapo Ugenini kucheza na Hull City ambayo ipo hatarini kuporomoka Daraja.
Hii ni nafasi safi kwa Liverpool kuzoa Pointi ikiwa wataweza kuisambaratisha Timu inayoongozwa na Nahodha wa zamani wa Manchester United, Steve Bruce, ambayo nayo inapigania kubaki Ligi Kuu England.
Lakini Liverpool Jana walipata habari mbaya baada ya Meneja wao Brendan Rodgers kutoboa kuwa Straika wao mkubwa, Daniel Sturridge, huenda asicheze tena Msimu huu akiwa bado hajapona matatizo ya Nyonga na Paja lake.
Msimu huu, Sturridge amekuwa nje kwa kipindi kirefu na kurejea tena na Mechi yake ya mwisho kushiriki ni ile ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP walipoitoa Blackburn Rovers hapo Aprili 8.
0 comments:
Post a Comment