Jumanne Usiku Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitaanza kwa Mechi mbili na moja ikiwa huko Jiji la Madrid, Spain ndani ya Estadio Vicente Calderon wakati Atletico Madrid watakapokuwa Wenyeji wa Mahasimu wao Real Madrid.
Mechi hii, Dabi ya Madrid, maarufu kama El Derbi MadrileƱo, ni Marudio ya Fainali ya Msim
u uliopita ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Real Madrid waliinyuka Atletico Madrid Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.
u uliopita ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Real Madrid waliinyuka Atletico Madrid Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.
Mechi nyingine ya Jumanne Usiku itachezwa huko Jiji la Turin Nchini Italy wakati Wenyeji Juventus watakapoivaa AS Monaco ya France.
MATCH REVIEW
Kila Timu itaingia kwenye Mechi hii ikidhamiria kisasi.
Kwa Atletico, kisasi chao ni kile cha kufungwa na Real kwenye Fainali ya Mashindano haya huko Lisbon Msimu uliopita na kwa Real ni kubondwa mara 4 na Sare 2 na Atletico tangu Fainali hiyo.
Vipigo kwa Real ni pamoja na kutupwa nje ya Spain Supercup na Copa del Rey.
Katika pambano lao la mwisho Mwezi Februari, kwenye Mechi ya La Liga, Atletico iliitwanga Real 4-0 ikiwa ndio ushindi wao mkubwa dhidi ya Wapinzani wao wakubwa katika Miaka 28.
Hilo limemfanya Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, aseme: "Matokeo ya mwisho na Atletico ndio yanatupa motisha sisi!"
Lakini, tofauti na Mechi zilizopita Msimu huu, safari hii Real watatinga kwa maadui zao Vicente Calderon wakiwa na Kikosi kamili kwa mara ya kwanza katika Miezi Mitano.
James Rodriguez na Toni Kroos, ambao waliikosa Mechi ya La Liga ya Jumamosi walipoifunga Eibar 3-0 baada ya kuwa Kifungoni, wanarejea dimbani.
Nao Atletico wana habari njema ya kurejea dimbani baada ya kuzikosa Mechi mbili akijiuguza Enka kwa Straika wao Mario Mandzukic ambae tangu ahamie Atletico akitoka Bayern Munich mwanzoni mwa Msimu amepachika Bao 20 zikiwemo Bao 2 katika Gemu mbili dhidi ya Real Uwanjani Vicente Calderon.
Jumatano pia zipo mechi mbili nyingine za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya PSG na Barcelona huko Mjini Paris na nyingine itachezwa huko Ureno kati ya FC Porto na Bayern Munich.
CREDIT:SOKA IN TANZANIA
0 comments:
Post a Comment