Kikosi cha Simba kimetamba kuendeleza wimbi la ushindi ili kiweze kiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.Hiyo imekuja baada ya Azam kuvutwa shati na Mtibwa Sugar juzi na kuambulia sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Manungu mjini Morogoro.Katika msimamo wa ligi kuu Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 baada ya kushuka dimbani mara 21.
Kocha Mkuu wa klabu hiyo Goran Kopunovic amesema bado wana matumaini ya kutwaa ubingwa kutokana na nafasi waliopo.
“Tupo katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa au kushika nafasi ya pili, tunafarijika kusikia wapinzani wetu (Azam) wanazidi kupoteza pointi muhimu kwao.,” alisema Goran.
Hata hivyo, aliongeza kuwa iwapo watashindwa kutwaa ubingwa basi watapambana kushika nafasi ya pili ili kushiriki mashindano ya kimataifa.
Simba imebakiza mechi tano ili kuhitimisha ligi hiyo na iwapo itashinda mechi zote, itafikisha pointi 50 wakati Azam itafikisha pointi 56 na Yanga pointi 61.
0 comments:
Post a Comment