Yanga wametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15 baada ya kuichapa Polisi Moro Bao 4-1 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu umewafikisha Pointi 55 huku wakibakisha Mechi 2 kumaliza Ligi na kufuatiwa na waliokuwa Mabingwa Azam FC ambao wana Pointi 45 na wamebakisha Mechi 3.
Shujaa wa Yanga ni Straika kutoka Burundi Amisi Tambwe aliepiga Hetitriki na Bao 1 kufungwa na anaeongoza Ufungaji Bora kwenye Ligi Simon Msuva ambae sasa amefikisha Bao 17 akifuatiwa na Amisi Tambwe mwenye Bao 14.
Kwa mjibu wa Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia mtandao wa twitter amepost
TFF leo imewapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa.Mh Dr Fennela Mukangara atawakabidhi kombe lao May
6 baada ya mechi yao vs Azam.
0 comments:
Post a Comment