Ligi Kuu England itaendelea tena Jumamosi na Manchester United wana nafasi ya kupanda hadi Nafasi ya Pili ikiwa wataifunga West Bromwich Albion Nyumbani Old Trafford.
Hivi sasa Man United wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal na Man City na Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wanahitaji kushinda Mechi 1 tu kutwaa Ubingwa.
Ushindi kwa Man United utawaweka Nafasi ya Pili, pengine kwa muda tu, kwa sababu Man City wanacheza Jumapili na Arsenal Mechi yao ipo Jumatatu.
Mbali ya Vinara Chelsea, ambao wanaweza kuwa Mabingwa Jumapili wakiifunga Crystal Palace, Man United, City na Arsenal, zikifuatiwa kwa mbali na Liverpool, Tottenham na Southampton, zinapigania kumaliza kwenye 4 Bora ili kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu huko The Hawthorns, WBA na Man United zilitoka 2-2.
MSIMAMO TIMU 4 ZA JUU
1. Chelsea Mechi 34 Pointi 80
2. Man City Mechi 34 Pointi 67
3. Arsenal Mechi 33 Pointi 67
4. Man United Mechi 34 Pointi 65
0 comments:
Post a Comment