Wakati Germany Bingwa tayari, Italy na England ikibaki toba tu, huko Spain ngoma bado mbichi zikiwa zimebaki Mechi 4 na Barcelona wakiongoza wakiwa Pointi 2 mbele ya Real Madrid na Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wakifuatia wakiwa Pointi 7 nyuma ya Real.
Mbali ya mbio hizo za Ubingwa, Masupastaa wa Timu hizi, Cristiano Ronaldo wa Real, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, na Lionel Messi wa Barcelona, wanafukuzana katika kuwania PICHICHI, Tuzo ya Mfungaji Bora wa La Liga, na hadi sasa Ronaldo yuko mbele akiwa na Bao 39 na Messi yuko nyuma kwa Bao 1.
0 comments:
Post a Comment