Pages

Tuesday, 5 May 2015

MKATABA WA IVO MAPUNDA UMEMALIZIKA SASA YUPO HURU KWENDA POPOTE


Wakati ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikielekea ukingoni, mlinda mlango wa Simba SC Ivo Mapunda anatarajiwa kumaliza mkataba wa kukitumikia kikosi cha ‘Wekundu wa Msimbazi’ ifikapo Mei 20 mwaka huu, lakini bado anamatumaini yakuendelea kubaki kwenye timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Mapunda amesema, mpaka sasa bado hajapata ‘ofa’ mpya ila yeye bado anaimani kuwa atapatiwa ofa na klabu hiyo na kama ikitokea timu yake isipofanya hivyo basi yeye atakuwa tayari kujiunga na timu yoyote itakayoonesha nia ya kutaka huduma yake.

“Mkataba wangu unaisha Mei 20 mwaka huu, bado sijapata ofa nyingine kutoka Simba wala klabu yoyote. Hapa ni nyumbani nafurahia kufanya kazi nikiwa Simba, nafanya kazi vilevile mpaka mkataba utakapo malizika wakihitaji kuniongezea mkataba mpya mimi nipo tayari”, amesema Mapunda.
Mpaka sasa hivi bado sijapata ofa yoyote, itategemea kama Simba wakiamua kunibakiza tutakuwa tumekubaliana vipi ila kwa sasa bado siko huru. Mkataba utakapo malizika basi nitajua nini kinafuata lakini niko tayari kwenda kufanya kazi kwenye timu yoyote itakayo nihitaji”, ameongeza Mapunda.

Kuhusu nafasi ya Simba kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili Mapunda amesema, nafasi bado ipo itategemea na Azam akiteleza itawapa wao nafasi. Lakini akaongeza kuwa, kwenye mpira chochote kinaweza kutokea na hiyo itategemea timu zilizobakiza mchezo na Azam zitacheza vipi, kama Azam itapoteza basi nafasi ya pili itakuwa ya Simba.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates