Arsenal wameichapa Hull City Bao 3-1 Ugenini huko KC Stadium hapo Jana na kuifikia Manchester City kwa Pointi na wao kubakia Nafasi ya 3 kwa tofauti ya Magoli lakini wao wana Mechi 1 mkononi.
Bao zote za Arsenal zilifungwa Kipindi cha Kwanza na Hull City kufunga lao Kipindi cha Pili.
Alexis Sanchez ndie alieipa Arsenal Bao la Kwanza katika Dakika ya 28 baada ya frikiki yake kumbabatiza Beki na kutinga.
Kisha Dakika ya 33 Shuti la Aaron Ramsey nalo lilimbabatiza Beki na kuandika Bao la Pili na Bao la 3 kufungwa Dakika ya 45 na Sanchez tena.
Dakika ya 56 Stephen Quinn aliipa Bao lao pekee kwa Kichwa na kuwafanya wafungwe 3-1 na kuporomoka na kushika Nafasi ya 4 toka mkiani.
MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA
0 comments:
Post a Comment