Julio amesema kwa takribani asilimia 99 amemalizana na Mwadui ambako atasaini mkataba wa miaka mitatu, lakini ameitwa na Coastal Union, hivyo anakwenda kuwasikiliza kesho jijini Tanga.
“Juzi nimetoka zangu Mwadui kufanya nao mazungumzo, kuna mambo mengi mazuri tumeongea nao kwa takribani asilimia 99. Coastal nao wameniita, naenda kuwasikiliza ni kitu gani wataniambia, baada ya hapo nitaongea kiundani ni wapi nimesimamia, lakini inavyoonekana nina nafasi kubwa ya kubaki Mwadui”. Julio ameiambia E-fm na kuongeza: “Mimi nitasema kile ambacho nimeongea na Mwadui, kibinadamu sio vizuri wenzio wanakuita, halafu unakataa kwa kujiona kama wewe ndio bora kuliko watu wote. Nakwenda kuongea nao kibinadamu, naenda kuwashukuru kwasababu nimefanya nao kazi salama”.CREDIT: MPENJA
0 comments:
Post a Comment