Tayari Bingwa ameshapatika, ambae ni Chelsea, na nyingine 3 zinazofuatia zitakazocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao zimeshapatikana na hizo ni Man City, Arsenal na Man United.
Pia, Timu 2 kati ya 3 ambazo zitashuka Daraja kucheza Ligi ya Championship Msimu ujao zimepatikana na hizo ni Burnley na QPR na Timu ya 3 kuungana nao itapatikana hiyo Jumapili na ni moja kati ya Newcastle au Hull City.
Hull, ambao wako Nafasi ya 3 toka mkiani wako Pointi 2 nyuma ya Newcastle lakini Hull wana tofauti ya Magoli Bora kupita Newcastle.
Kila Timu inahitaji ushindi hiyo Jumapili maana ikiwa Newcastle itatoka Sare na West Ham watakapocheza Uwanjani Saint James Park, Nyumbani kwa Newcastle, na Hull City, ambao wako Nyumbani KC Stadium, wakiifunga Man United, licha ya sasa kufungana Pointi, basi Hull watapona na Newcastle kushushwa.
Timu zote hizo, Hull na Newcastle, zinacheza na Wapinzani ambao hawana cha maana kwenye Mechi zao mbali ya kukamilisha Ratiba tu.
Lakini Steve Bruce, Meneja wa Hull ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United, anajua fika nini ugumu wa kuifunga Man United maana katika Mechi 21 alizocheza dhidi ya Man United katika Miaka 17 ya kazi yake ya Umeneja hajawahi kuifunga Man United hata mara moja.
0 comments:
Post a Comment