Jana Usiku, Peru wamefanikiwa kutwaa ushindi wa 3 wa Kombe la Mataifa ya Amerika ya Kusini, Copa America, hii ikiwa ni mara yao ya pili mfululizo, baada ya kuwachapa Paraguay 2-0 huko Estadio Municipal Alcaldesa Ester Roa Rebolledo, Jijini ConcepciĆ³n Nchini Chile.
Bao zote za Peru zilifungwa Kipindi cha PIli na Andre Carrillo na Paolo Guerrero.
Leo Usiku, huko Estadio Nacional de Chile Jijini Santiago Wenyeji Chile watacheza na Argentina katika Fainali ya Copa America huku Chile wakisaka kubeba Kombe lao la kwanza katika Historia yao wakati Argentina wakisaka Taji la kwanza baada ya Miaka 22.
Timu hizi zinatinga Fainali hii zikiwa na Historia tofauti lakini wote wanahaha kufuta ukame wao wa Mataji.
Argentina, wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani mara 4 Lionel Messi, ambao Mwaka Jana walifungwa na Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil, hawajatwaa Kombe lolote kwa Miaka 22 baada ya kutwaa Copa America.
Hali hii imemfanya Kepteni Lionel Messi, ambae ana mafanikio makubwa yasiyo na mfano kwenye Klabu yake FC Barcelona ya Spain, azungumze: "Kizazi hiki kinahaha kutwaa Taji na Timu ya Taifa. Kama Timu tunastahili kushinda kitu hasa baada ya kuwa karibu mno kutwaa Kombe la Dunia!"
Kikosi cha Argentina kimesheheni Mastaa wakubwa wanaojulikana Dunia nzima wakiwemo Sergio Aguero, Javier Mascherano, Angel Di Maria, Carlos Tevez na Gonzalo Higuain.
Lakini Miaka nenda rudi wako kapa na Aguero, anaechezea Manchester City, amesisitiza: "Kama kizazi hiki hatutashinda lolote, basi tutajuta maisha yetu yote!"
Argentina, maarufu kwa jina la La Albiceleste, wakishinda Fainali hii wataungana na Uruguay kwa kubeba Copa America mara 15 ambazo ni mara nyingi kupita Taifa lolote huko Marekani ya Kusini.
Tofauti na La Albiceleste, Wenyeji Chile, maarufu kwa jina la La Roja wenye majina maarufu machache, yale ya Alexis Sanchez na Arturo Vidal, Leo wana Mlima mrefu mno kuupanda.

0 comments:
Post a Comment