Pages

Saturday, 4 July 2015

MMISRI WA CHELSEA ALIYEIUA TAIFA STARS KUSHTAKIWA NA FIORENTINA

Klabu ya Italy Fiorentina inatafakari kumchukulia hatua za kisheria Winga wa Chelsea Mohamed Salah ambae amegoma kurudi kwenye Klabu hiyo kwa ajili ya Kipindi cha pili cha Mkopo wake.
Salah, Mchezaji kutoka Egypt mwenye Miaka 23, alihamia kwa Mkopo Fiorentina Januari Mwaka huu huku akitoboa wakati huo kuwa Mkopo huo unaweza kurefushwa na kuongezwa Msimu wa pili.

Lakini Fiorentina sasa imedai Salah anataka kujiunga na Klabu nyingine baada ya kuukataa Mkataba mpya ulioboreshwa na pia kugomea kurudi mazoezini kwa ajili ya Msimu mpya.
Fiorentina imesema suala hilo sasa liko kwa Wanasheria wao.
Akiwa na Fiorentina kwa Mkopo, Salah alicheza Mechi 26 na kufunga Bao 9 na alijiunga na Chelsea Mwaka uliopita kutoka FC Basel ya Uswisi kwa Dau la Pauni Milioni 11 lakini alicheza Mechi 19 tu na kuanza Mechi 6 za Ligi Kuu England ndipo akatolewa kwa Mkopo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates