Pages

Saturday, 4 July 2015

STARS YATOLEWA KUFUZU CHAN BAADA YA KUTOKA SARE YA 1-

Taifa Stars Leo huko Nakivubo, Kampala imetoka Sare 1-1 katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CHAN 2016 kuwania kucheza Fainali Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani ya Nchi zao huko Rwanda Mwakani lakini imetupwa nje ya Mashindano hayo.
Matokeo hayo yameifanya Uganda isonge Raundi ijayo kwa Jumla ya Mabao 4-1 kwani walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Amaan Stadium, Zanzibar Wiki mbili zilizopita Bao 3-0 na huo ukawa mwisho wa Kocha wa Stars, Mart Nooij, na badala yake TFF ikamteua Charles Boniface Mkwasa.

Kwenye Mechi hii ya Leo, katika Dakika ya 17 Taifa Stars, walioonekana wazuri na wachangamfu, walifunga Bao baada ya Krosi ya Rashid Mandawa kuunganishwa na John Bocc lakini Refa alilikataa Bao hilo kwa Ofsaidi.
Hadi Mapumziko Gemu ilikuwa 0-0.
Star walipata Bao lao kwa Penati ya Dakika ya 58 iliyopigwa kifundi na John Bocco lakini Uganda wakasawazisha Dakika ya 82 kupitia Kizito Kezironi alieingizwa punde tu kutoka Benchi.
Bao hizo zilidumu hadi Dakika ya 90 Mpira ulipomalizika.
Uganda sasa wamesonga Raundi ijayo na watakutana na Sudan na Mshindi wa Mechi hiyo atatinga Fainali huko Rwanda.
VIKOSI:
Uganda Cranes: James Alitho, Denis Okot Oola, Brian Ochwo, Hassan Waswa Mawanda, Shafiq Bakaki, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu, Farouk Miya, John Semazi, Robert Sentengo
Taifa Stars: Ally Mustafa " Barthez", Shomary Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo "Chumvi", John Bocco, Rashid Mandawa, Saimon Msuva
Akiba: Mudathir Khamis, Juma Abdul, Hassan Isihaka, Salum Telela, Said Ndemla, Ramadhani Singano, Ame Ally
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates