Kocha Sylvester Marsh amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marsh alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, hali ya Marsh aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Kilimanjaro Stars pia alizinoa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara iliendelea kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele.
Pamoja na hivyo suala la afya yake liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka kutafuta wodi aliyolazwa.
Aliwahi kuugua taabani na kukawa na taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini baadaye lilikanusha.
Mdau, Abdulfatah Saleh ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ndiye alijitolea kumhudumia katika matibabu yake.
source :saleh jembe
0 comments:
Post a Comment