Pages

Saturday, 14 March 2015

SIMBA UKAWA KUIPIGIA YANGA KIDEDEA WATAKAPOUMANA NA PLATINUM

Baada ya uongozi wa Yanga kuwaomba mashabiki wa klabu tofauti za hapa nchini kujitokeza na kuwapa sapoti kwenye mchezo wao wa kesho Jumapili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe, mashabiki wa Simba wa Tawi la Mpira na Maendeleo, maarufu kwa jina la Simba Ukawa, wamekubali kufanya hivyo ila wakatoa masharti.
Yanga, kesho inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kucheza na Platinum, 
Mwenyekiti wa tawi hilo, Mohammed Kingolile, amesema kuwa wao linapokuja suala la klabu kuiwakilisha nchi, huwa hawana kinyongo na Yanga, hivyo wapo tayari kuishangilia kwa nguvu zote.
“Tupo tayari kuwashangilia lakini kauli za kuikejeli Simba alizozitoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu yao, Jerry Muro, kabla ya mchezo wetu dhidi yao wiki iliyopita, zimetufanya kusita kuishangilia mpaka pale watakapotuomba radhi.”

SOURCE: CHAMPIONI JUMAMOSI.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates