Kocha wa Arsenal Arsene Wenger huenda akawa kwenye wakati mgumu baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade Chamberlain
Chamberlain hatakuwepo kwa takriban wiki tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Kulingana na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa Arsenal kuimarisha ambao wanataka kujiweka pazuri katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya tatu .
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi tarehe 4.
SOURCE: BBC
0 comments:
Post a Comment