Pages

Friday, 13 March 2015

MCHEZAJI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED DIEGO FORLAN ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Manchester United,Atletico Madrid,Intermilan Diego Forlan jana ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay baada ya kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2002.
Forlan,35, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Cerezo Osaka ya nchini Japan amekuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Uruguay na mwaka 2010 aliiwezesha timu hiyo kushinda nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko nchini Afrika kusini huku yeye akibeba tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo baada kuonesha kiwango bora.
“Ninawashukuru kwa wote walionipa ushirikiano tangu naanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002, ninaamini timu itaendelea kufanya vizuri na nimechukua uamuzi huu ili kutoa kwa nafasi kwa wachezaji wengine ambao ninatumaini wataisadia timu hii” alisema Forlan.
Mchezaji huyo aliyepata sifa nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu mpaka anatangaza kustaafu tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uruguay michezo 112 na kufunga magoli 36.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates