Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba, kimeendelea kuitesa Yanga, hiyo ni baada ya jana asubuhi kufanyika kikao kizito kati ya viongozi wote wa matawi wa Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kisha kutolewa maoni ‘tata’.
Kikao hicho, kilifanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga kikiongozwa na Sanga na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ambacho wanachama walidai uwepo wa wachezaji wasio na mapenzi, wakiwemo kutoka Simba, unaweza kuwafanya wacheze bila kujituma.
Sanga amesema katika kikao hicho, viongozi hao wa matawi wameuomba uongozi kufanya uboreshaji wa usajili wao msimu ujao baada ya kutokea minong’ono mingi juu ya hujuma hizo.
Hivi karibuni, kuliibuka maneno kuwa, kuna baadhi ya wachezaji ambao walitua klabuni hapo wakitokea Simba, hawana moyo wa kujituma kama wengine, madai ambayo uongozi wa Yanga umeyakanusha.
Wachezaji waliopo Yanga ambao waliwahi kuitumikia Simba ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondani, Danny Mrwanda, Deogratius Munish ‘Dida’, Amissi Tambwe na Mrisho Ngassa.
SOURCE:SALEH JEMBE
0 comments:
Post a Comment