Pages

Friday, 13 March 2015

TIMU 4 ZAINGIA ROBO FAINALI UEFA HATMA YA TIMU ZA UINGEREZA KUJULIKANA WIKI IJAYO

PSG na Bayern Munich Jumatano Usiku zimeungana na Mabingwa Watetezi Real Madrid na FC Porto kwenye Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na kubakiza machungu makubwa kwa Jose Mourinho na Chelsea yake ambayo ilitupwa nje na Mtu 10 PSG.
PSG, wakicheza Mtu 10 kwa zaidi ya Saa 1 na Nusu baada ya Staa wao Zlatan Ibrahimovic kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya kwa Oscar, walitoka Sare 2-2 na Chelsea na kusonga kwa Bao za ugenini kwa vile Mechi yao ya kwanza iliisha kwa Sare 1-1.
Wiki ijayo, Timu nyingine 4 zitakamilisha safu ya Robo Fainali ya UCL ambayo Ratiba yake itajulikana hapo Machi 20 lakini ipo hatari kubwa England ikakosa hata Timu moja hatua hiyo.
Wiki ijayo, kama vile kwa Chelsea, Arsenal na Man City, zipo hatarini kuyavaa machungu ya Mourinho baada ya zote kutandikwa kwao Mechi za kwanza.
Wiki ijayo, Arsenal wako huko France kurudiana na AS Monaco, Timu ya zamani ya Meneja wao Arsene Wenger, ambayo iliichapa Arsenal 3-1 kwao Emirates katika Mechi ya kwanza.
Wiki ijayo, Man City ina kazi ngumu mno huko Nou Camp Jijini Barcelona watakapojaribu kupindua kipigo cha 2-1walichopewa kwao Etihad na FC Barcelona.
Wiki ijayo, hatima ya England kuwepo Ulaya kwenye Mashindano makubwa ya Klabu itajulikana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates