Pages

Thursday, 12 March 2015

KOCHA WA POLISI MORO ATIMULIWA NAE DENNIS KITAMBI KOCHA WA ZAMANI WA NDANDA APATA MCHONGO AZAM FC


Baada ya sare katika mchezo dhidi ya Ruvu shooting hapo jana, uongozi wa Polisi Morogoro umemsimamishia mkataba kocha wake Adolph Richard kama mkataba walio inga unavyo eleza.

Adolph Richard ambaye ameipandisha Polsi Morogoro ligi kuu alikuwa jukwaani wakati vijana hao wa Morogoro wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya mchezo unao fuata wa ligi kuu ya vodacom.
Adolph akizungumza na moja ya kituo cha redio nchini amesema kuwa amesitishiwa mkataba na uongozi kutokana na mkataba ailiyokuwa ameingia na timu hiyo, ambapo ulikuwa unaeleza kuwa akipoteza michezo mitatu mfululizo, uongozi unahaki wa kujadili na kumsimamisha.

Polisi Morogoro umepoteza michezo mitatu mfululizo, ambayo ni dhidi ya Simba SC, Kagera Sugar na Mtibwa sugar na hapo jana kuhitimsha safari yake kwa sre ya bila kufungana na Ruvu shooting, na uongozi kuamua kumsitisha mkataba, kama mkataba unavyoeleza.

Msemaji wa Plosi Morogoro amethibitisha kusitishwa kwa kocha huyo, ambapo amesema kuwa uongozi umefikia uwamuzi huo, baada ya timu kuwa na matokeo mabovu katika siku za karibuni.


DENNIS KITAMBI KOCHA MSAIDIZI AZAM
Aliyekuwa kocha wa Ndanda FC Denis Kitambi ameanza kibarua chake kipya ndani ya Azam FC baada ya kuwa nnje katika tasnia ya ukocha kwa takribani miezi 5, toka Uongozi wa Ndanda FC kuamua kuachana nae baada ya kuwa na matokeo mabovu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo wekwa katika ukurasa wa Azam FC, Kitambi anaingia Azam FC kama kocha msaidizi na leo ameanza kazi.
"Dennis Kitambi, kocha wa zamani wa Ndanda FC na mchambuzi wa soka kwenye luninga leo ameanza kazi kama kocha msaidizi wa George Best Nsimbe", ilieleza taarifa hiyo iliyowekwa katika ukurasa wa Azam FC.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates