Pages

Wednesday, 11 March 2015

UEFA LEO USIKU VITA KALI CHELSEA VS PSG HUKO ALLIANZ ARENA BAYERN NAO DIMBANI KUWAWINDA DONETSK

Chelsea FC v Paris Saint-Germain
Leo Uwanjani Stamford Bridge Jijini London, Chelsea watakuwa Wenyeji wa Paris St Germain katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi ya kwanza huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France hapo Februari 17,Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea Bao muhimu la Ugenini walipotoka Sare 1-1 na PSG.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza na kushinda 2-0 Uwanjani Stamford Bridge huku Bao lao la pili likipachikwa mwishoni na Demba Ba katika Dakika ya 87.
Wakati Chelsea inatarajia kumrudisha Kikosini Kiungo wao Nemanja Matic ambae hajacheza tangu atumikie Kifungo cha Mechi mbli alichopewa baada ya kufungiwa kutokana na Rafu mbaya kwenye Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley Mwezi uliopita, David Luiz wa PSG anatarajiwa kurudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge tangu aihame Chelsea mwanzoni mwa Msimu.
David Luiz, Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, alipozongwa na Wanahabari kuelezea kuhusu Meneja wake wa zamani hasa kuhusu Lebo ya Meneja huyo wa Chelsea Jose Mourinho kupachikwa ni ‘Mtu Spesho’ alijibu: “Ni spesho kwenu si kwangu!”

FC Bayern München v FC Shakhtar Donetsk
Bayern Munich wako kwao Allianz Arena Jijini Munich, Germany, kurudiana na FC Shakhtar Donetsk baada ya Sare yao ya 0-0 huko Nchini Ukraine katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Bayern watatinga kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri, Xabi Alonso Mchezaji wa Kimataifa wa Spain, ambae yupo Kifungoni baada ya kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi yao ya kwanza baina ya Timu hizi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates