Pages

Sunday, 15 March 2015

YANGA WAIUA PLATINUM TAIFA YASHINDA 5-1 NGASA ATUPIA MBILI

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho Yanga, wamefanikiwa kuwachapa goli 5-1 FC Platinum ya Zimbabwe na kutengeneza mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo.



Yanga SC wakicheza katika uwanja wa Taifa bila ya nahodha wao Nadir Haroub 'Cannavaro' waliuwanza mchezo huo kwa kasi na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga na kushindwa kuzitumia katika dakika 30 za mwanzo, ambapo FC Platinum wakiwa wakitumia mashambulizi ya kushtukiza.

Yanga walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa kiungo Salim Telela katika dakika ya 31 ya mchezo goli lililodumu kwa dakika 12 kabla ya Haruna Niyonzima kuipatia yanga goli la 2 akitumia vyema pasi ya Ngassa katika dakika ya 43.

Wakati yanga wakijiandaa kwenda mapumziko FC Platinum waliandika goli lao la kwanza na pekee katika mchezo huo katika dakika ya 45 kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja hadi kwenye nyavu za yanga, na kupelekea mchezo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-1.

Kipindi cha pili yanga sc walirejea kwa kasi na katika dakika ya 46 Amisi Tambwe akitumia mpira wa Mrisho Ngassa aliipatia yanga goli la 3, kabla ya Ngassa kuiandikia yanga goli la 4 katika dakika ya 51 ya mchezo.

Wakati mchezo ukionekana kuanza kubalance Mrisho Ngassa alihitimisha kalamu ya magoli kwa kuifungia Yanga goli la 5 katika dakika ya 88 akitumia vyema pasi Kpah Sherman na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 5-1. 

Kwa matokeo hayo ya leo yanawafanya yanga kuwa katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho ambapo katika mchezo wa marejeano utakao chezwa baada ya wiki mbili yanga wanatakiwa kupata sale ya aina yoyote ile na wala wasikubali kufungwa jumla ya magoli 4-0 katika mchezo wa marejeano.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates