Borussia Dortmund wametinga Fainali ya Kombe la Germany, DFB-POKAL, baada ya kuwabwaga Mabingwa Watetezi Bayern Munich kwa Penati 2-0 kufuatia Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Gemu iliyochezwa Nyumbani kwa Bayern, ndani ya Allianz Arena.
Kwenye Fainali, Borussia Dortmund, ambao mwishoni mwa Msimu wanamuaga Kocha wao Jurgen Klopp, watacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine inayochezwa Leo kati ya Timu ya Daraja la 3 Arminia Bielefeld na Klabu ya Bundesliga, VfL Wolfsburg.
Katika Nusu Fainali hii, Bayern walitangulia kufunga Bao la Dakika ya 29 la Robert Lewandowski na Dortmund kurudisha Dakika ya 75 kwa Bao la Mchezaji kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Dortmund walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Kampl kupewa Kadi Nyekundu lakini mwisho Bao zilibaki 1-1.
Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Bayern walikosa Penati zao zote 4 zilizopigwa na Xabi Alonso, Philipp Lahm, Mario Gotze na Kipa Manuel Neuer huku Dortmund wakifunga 2 kupitia Sebastian Kehl na Ilkay Gundogan.

0 comments:
Post a Comment