Vinara wa La Liga FC Barcelona Jana Usiku wameishindilia Getafe Bao 6-0 na kupanda na kuwa mbele ya Timu ya Pili Real Madrid kwa Pointi 5.
Hadi Mapumziko Barca, waliocheza kwao Nou Camp, walikuwa mbele kwa Bao 5-0.
Mabao hayo ya Mafowadi wa Barca, Messi, Suarez na Neymar yamewafikisha zaidi ya Bao 100 kwa Msimu huu kwa Timu yao.
Hii Leo, Real Madrid watacheza na Almeria Uwanjani Santiago Bernabeu.
Katika zile mbio za kugombea Ufungaji Bora na kutwaa Tuzo ya Pichichi ambazo hivi sasa Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo ndie yupo Nambari Wani akiwa na Bao 39 na Messi sasa kumkaribia akiwa Bao 1 nyuma.
MSIMAMO TIMU 5 ZA JUU
**Kila Timu imecheza Mechi 33 isipokuwa inapotajwa.
1. Barcelona Mechi 34 Pointi 84
2. Real Madrid 79
3. Atletico Madrid 72
4. Valencia 68
5. Sevilla 66
0 comments:
Post a Comment