Pages

Wednesday, 29 April 2015

MANCHESTER UNITED KUCHEZA NA BARCELONA KATIKA ZIARA YAO MAREKANI


Manchester United wataivaa Barcelona ikiwa ni moja ya Mechi zao 4 huko Marekani kwenye Ziara yao ya kabla Msimu mpya wa 2015/16 kuanza.
Man United, Mabingwa wa England mara 20,watacheza na Barca ndani ya Levi's Stadium Mjini Santa Clara, California, hapo Julai 25.
Mechi hizi ni za Mashindano ya International Champions Cup ambayo Mwaka Jana, wakiwa chini ya Kocha mpya Louis van Gaal, Man United iliitwanga Liverpool 3-1 kwenye Fainali na kubeba Kombe.

Kwenye Fainali hiyo, Liverpool walitangulia kwa Penati ya Steven Gerrard lakini Man United wakajibu kwa Bao 3 za Wayne Rooney, Juan Mata na Jesse Lingard.
Kwa kuelekea Fainali, Man United walizibwaga Klabu za Italy, AS Roma na Inter Milan, na kisha kuitwanga Real Madrid.
Mechi nyingine za Man United ni huko Chicago hapo Julai 29 dhidi ya Paris St Germain na kisha dhidi ya Klabu ya Mexico, Club America, watakayocheza Mjini Seattle na ile ya Klabu ya Marekani, San Jose Earthquakes, watakayocheza kwenye Uwanja utakaotangazwa baadae.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

IDADI YA WANAOTEMBELEA BLOG HII

Blog Archive

Recent Posts

Fashion

3/Fashion/big-col-right

Recent Posts

Header Ads

Followers

Powered By Blogger

Tags

Maoni

3/recent-comments

WASILIANA NASI

Popular Posts

Labels

Blog Archive

Blogger templates