Bosi wa Brendan Rodgers amesema Fowadi wa Liverpool Raheem Sterling hataondoka mwishoni mwa Msimu licha ya mazungumzo ya Mkataba mpya kati take na Klabu kuvunjika.
Juzi Sterling, Kijana wa Miaka 21, akifanya Mahojiano na BBC, alisema kuukataa Mkataba mpya ambao ungemlipa Pauni 100,000 kwa Wiki badala ya 35,000 za sasa si uroho was Fedha Bali nia take yeye no kutwaa Mataji.
Zipo ripoti kuwa Sterling yuko mbioni kuhamia Barcelona au Real Madrid za Spain lakini pia habari hizo zimegusia kubaki kwake England Ila atahamia Chelsea au Arsenal.
Hapo Jana Brendan Rodgers amesema: "Liverpool no Mona ya Supapawa za Soka. Wamiliki wakisema hauzwi Mchezaji, basi hauzwi!"
Katika Mkataba wake was sasa na Liverpool, Sterling amebakisha Miaka Miwili.
Rodgers pia alisema Raheem, ambae alijiunga na Liverpool 2010 akitokea QPR, hakuruhusiwa kufanya Mahojiano na BBC lakini atajifunza kutokana na makosa take.
Pia Wachambuzi wengi was Soka huko Uingereza wameibuka na kumtaka Sterling abakie Liverpool kwani hajakomaa Kisoka kwenda nje.
0 comments:
Post a Comment